Chama cha TPLF kwenye eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, kimeituhumu serikali kuu kwa kujaribu kuficha kile imesema muendelezo wa mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu, huku pia kikidai Addis Ababa inazorotesha kwa makusudi utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Pretoria.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa iliyotolewa na TPLF, serikali  imekwamisha utelekezaji wa mkataba wa Pretoria na kuendelea na mauaji ya kimbari dhidi ya watu  wao huku maafisa wa kiraia na kijeshi wakishirikiana kupunguza au kuficha ukubwa wa janga la kibinadamu kwenye eneo hilo.

Chama hiki kinasema kuwa idadi kubwa ya wakimbizi  ni watoto pamoja na wazee ambao wapo katika hali mbaya kutokana na njaa na magonjwa na kwamba hali itazorota zaidi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.

Katika barua iliyotumwa wiki iliyopita kwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, TPLF imedai kuwa  baada ya miaka mitano ya mauaji ya tangu Novemba 2020, kiwango cha vifo kimeongezeka mwezi Desemba mwaka jana.

Aidha TPLF imesema vituo vya watu waliokimbia makazi yao katika maeneo ya Hisats, Shire, Adwa, Abiy-Addi, Adigrat na Mekelle vinakabiliwa na kile ilichokiita dhulma za ubinadamu, raia wakinyimwa mahitaji muhimu kwa makusudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *