Kuelekea kuanza kwa muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2026 baadhi ya wazazi na walezi huko mkoani Tabora ambao wapo katika maandalizi ya kuwanunulia vifaa vya masomo watoto wao wamelalamikia hali ya ongezeko la bei ya vifaa mbalimbali vya shule na kusababisha baadhi yao kushindwa kumudu gharama za mahitaji hayo muhimu.
Harakati za kuwarudisha wanafunzi shuleni zikiwa zinaendelea karibu kila kona hapa nchini huko mkoani Tabora imeshuhudiwa kwenye masoko mbalimbali ikiwemo soko kuu Tabora mjini wazazi na walezi wakijitokeza kufanya maandalizi ya manunuzi ya vifaa vya shule kwa ajili ya watoto wao.
#KilichoBoraKabisa