Kocha Ettiene Ndayiragije amewapongeza Yanga kwa kuwapa mchezo mgumu lakini amewapa kongole wachezaji wake kwa kufuata maelekezo na kuonyesha kiwango bora licha ya kupoteza bao 1-0.

Ettiene amegusia suala la timu hiyo kuendelea kuwa bora siku hadi siku pamoja wachezaji kuonyesha kufanyia kazi changamoto kama vile utengenezwaji wa nafasi na kadhalika.

Ameshukuru pia mualiko wa michuano hii ya Mapinduzi 2026 kwani ameweza kupata muda zaidi wa kukaa na kuielewa timu na kutengeneza muunganiko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *