Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesema imetenga zaidi ya Bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu na mazingira ya utoaji elimu na ujifunzaji kwa ajili ya muhula wa masomo wa mwaka 2026 unaotarajiwa kuanza Jumanne, Januari 13, 2026.

Wakizungumza na wakuu wa shule na wasimamizi wa taaluma kwa shule za msingi na sekondari zilizopo jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya wamesema ni muhimu viongozi wa shule hizo kutimiza wajibu wao ili dira ya ya kuwa kinara wa ubora wa elimu na ufaulu kwa halmashauri hiyo iweze kutimizwa.

Mhariri @Moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *