Maelfu ya wananchi wa wa Colombia wamefanya maandamano nchi nzima kulaani vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yao kama vile vya kuishambulia kijeshi Venezuela.

Maandamano hayo yamefanyika katika miji ya Medellin, Cucuta na katika mji mkuu wa Colombia, Bogota wakiitikia wito wa Rais wa nchi hiyo Gustavo Petro aliyataka wananchi kufanya maandamano ya kitaifa ili kutetea mamlaka ya kujitawala nchi hiyo. 

Huku wakipeperusha bendera za Colombia, waandamanaji wamepiga nara na shaari “Dumu daima dawamu Colombia iliyo huru”. Aidha wamepiga nara: “Marekani ni tishio kuu kwa amani ya dunia.” Wamerekani rudini kwenu,” na “Petro hayuko peke yake.” 

Mwandamanaji mmoja huko Bogota amesikika akisema: Trump ni rais wa vita na ameitaka Kongresi ya Marekani kuchukua hatua za kumvua urais.

Jumapili iliyopita Trump alimtaja Rais wa Gustavo Petro wa Colombia ambaye anamtuhumu kuwa anahusika katika biashara ya mihadarati kuwa “mtu mgonjwa.”

Rais wa Marekani aidha alipendekeza kuwa uvamizi wa kijeshi dhidi ya Colombia, ambayo ina akiba kubwa ya mafuta kama Venezuela, “ni jambo linalosikika vizuri kwake”.

Rais wa Colombia hakubakia kimya mkabala wa tuhuma za Truump na ametahadharisha kuwa “atabeba silaha” mwenyewe ikiwa Marekani itaanzisha hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya nchi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *