Wizara ya Afya inaendelea kutoa huduma maalum za upasuaji kwa wagonjwa wa mabusha, Katika Kituo cha Afya Kinondoni, Dar es Salaam.

Farasi wa #MorningTrumpet amefika kituoni hapo na kuelezwa kuwa, huduma hiyo ya upasuaji imekuwa ikitolewa kuanzia Januari 5 na itaendelea hadi Januari 30 katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo waathirika wamepata matibabu ya kitaalamu bila gharama.

Ugonjwa wa mabusha husababishwa na maambukizi ya minyoo aina ya filarial worms wanaoenezwa na mbu wa jamii ya Culex. Ugonjwa huo husababisha kujaa maji kwenye korodani na kuathiri afya na maisha ya wagonjwa.

✍Roland John
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *