#HABARI: Hali ya simanzi na hasira vimetawala katika Kata ya Itetemia, Wilayani Tabora, kufuatia kifo cha kusikitisha cha mtoto Yasin Sadiki (3), aliyepoteza maisha baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji ya mvua yaliyotuama katika shimo la kuchimba mchanga.

Tukio hilo ambalo limeibua taharuki na hasira miongoni mwa wananchi walioshuhudia, ambapo kundi la watu wenye hasira liliishinikiza kutaka kuchoma moto gari la mtu anayedaiwa kuwa mmiliki wa eneo hilo. Wananchi hao wanadai kuwa mmiliki huyo amekuwa akijinufaisha kwa kuchimba mchanga na kuliacha eneo hilo likiwa wazi bila kuweka uzio wala tahadhari yoyote kwa watoto na wapita njia.

Wakizungumza kwa uchungu katika eneo la tukio, wananchi wameeleza kuwa hili si tukio la kwanza kutokea na wameiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wamiliki wa machimbo ambao hawaheshimu kanuni za usalama.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *