#HABARI: Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia mbili na tisini (Tsh 290,000,000) kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Fedha hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya robo ya pili ya mwaka wa fedha kwa ajili ya kutoa mikopo ya kimaendeleo kwa makundi hayo maalum.
Akikabidhi hundi za fedha hizo kwa vikundi hamsini na tano (55) vya walengwa, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Christopha Maghala, amewataka wanufaika, hususan waliokuchukua mikopo ya kilimo, kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa. Amewahimiza kutumia mvua chache zilizopo kupanda mazao yanayokomaa mapema ili kuhakikisha wanapata mavuno bora na kuweza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.