#HABARI: Meneja wa Uwakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Katavi Mhandisi Innocent Mlay, amesema kuwa Mkoa wa Katavi umejipanga kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya miundombinu, ili kukabiliana na mvua ambazo zimeanza kunyesha tangu Novemba mwaka 2025.
Mhandisi Mlay ameeleza kuwa katika kutekeleza hilo wamejipanga kukagua barabara, mifereji, madaraja na makalavati, ili kuhakikisha endapo kuna uchafu au mchanga umejaa unaondolewa mapema, ili kuzuia mafuriko na kuruhusu maji kupita kwenye njia yake.
Aidha, amebainisha kuwa Mkoa wa Katavi umejitahidi kufungua barabara mpya nyingi, ili kufika maeneo ambayo awali hayakuwa yakifikika.
Mhandisi Mlay amesema kuwa hivi sasa wananchi wanashuhudia mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kutokana na maboresho hayo tofauti na zamani, ambapo madalali pekee ndio walioweza kufika mashambani na walikuwa wakipanga bei za mazao kwa wakulima, lakini sasa hivi wakulima wenyewe wanauza mazao yao moja kwa moja na kupanga bei kulingana na uzalishaji wao, jambo linalowapa faida kubwa na kuboresha maisha yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania