Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu ameagiza kuvunjwa mara moja kwa mkataba wa kampuni ya Bugeta Engineering Ltd kwa kushindwa kutekeleza kwa wakati mradi wa ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo, Naibu Waziri amesema ucheleweshaji wa kazi umeathiri moja kwa moja mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, jambo lisilokubalika kwa Serikali inayolenga kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

✍ Mawazo Mwaijengo
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *