Ubalozi wa Marekani nchini Iran siku ya Jumatatu umetoa taarifa mtandaoni ya onyo la usafiri ikiwataka raia wa Marekani kuondoka Iran mara moja huku machafuko yakiendelea kusambaa kote nchini humo.
“Raia wa Marekani wanapaswa kutarajia kuendelea kuminywa kwa intaneti, kupanga njia mbadala za mawasiliano, na, ikiwa ni salama kufanya hivyo, kufikiria kuondoka Iran kwa njia ya ardhini hadi Armenia au Uturuki,” ilisema ubalozi huo mtandaoni katika taarifa kwenye tovuti yake.
Pia iliongeza kuwa raia wenye uraia mara mbili wa Marekani na Iran lazima waondoke Iran kwa pasipoti za Iran kwani serikali ya Iran haitambui uraia pacha.
“Raia wa Marekani wako katika hatari kubwa ya kuhojiwa, kukamatwa, na kuwekwa kizuizini nchini Iran,” Taarifa hiyo ilisema.
Kulingana na taarifa hiyo, mashirika ya ndege yanaendelea kupunguza au kufuta safari za ndege kwenda na kutoka Iran, huku huduma kadhaa zikisimamishwa hadi Ijumaa.
#kilichoborakabisa
