Kutokana na kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza nchini yanayoendelea kuathiri nguvu kazi ya Taifa, Watanzania wameshauriwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao badala ya kusubiri mpaka waugue.
Mkurugenzo Mtendaji wa Kampuni ya Norland Global Tanzania, Dkt Moses Makalla amesema
ni muhimu kuchukua hatua za kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa dalili zake hazijitokezi mapema.
Norland Global ni kampuni inayojihusisha na utafiti, utengenezaji na utoaji wa tiba kwa magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza yenye makao makuu nchini China ikitoa huduma za matibabu duniani kote kwa kutumia bidhaa za asili zilizofanyiwa tafiti za kina na kuthibitishwa na taasisi za afya za kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2020, magonjwa yasiyoambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41, sawa na asilimia 71 ya vifo vyote duniani, ikilinganishwa na milioni 57 vilivyoripotiwa mwaka 2016. Tanzania, magonjwa hayo yanachangia asilimia 33 ya vifo vyote.
Amesema magonjwa yanayowaathiri Watanzania wengi ni pamoja na kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya figo, homa za ini, upungufu wa damu, tindikali tumboni pamoja na vidonda vya tumbo.
# starTvUpdate
