Meli ya mafuta iliyokamatwa na Marekani katika Atlantiki Kaskazini wiki iliyopita imepelekwa Scotland kuchukua bidhaa mpya, serikali ya Uingereza imesema.
Marekani imeishutumu meli hiyo kwa kuvunja vikwazo kwa kubeba mafuta kwa ajili ya Venezuela, Urusi na Iran.
Meli hiyo, ambayo hapo awali ilijulikana kama Bella 1, ilipatikana ikiwa kusini mwa Iceland katika operesheni iliyoungwa mkono na vikosi vya Uingereza.
Meli ya Marinera iko katika eneo lililohifadhiwa la bahari kati ya pwani ya mashariki ya Nyanda za Juu na pwani za Moray na Aberdeenshire – pamoja na meli zinazotumika kuvuta zingine na za Walinzi wa Pwani ya Marekani.
Msemaji wa serikali ya Uingereza alisema: “Meli ya Bella 1 iliingia majini Uingereza ili kujazwa vifaa muhimu – ikiwa ni pamoja na chakula na maji kwa wafanyakazi – mapema leo kabla ya kuendelea na safari yake.”
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) ilisema “kuzuia, kuvuruga na kudhalilisha” meli za Urusi ilikuwa kipaumbele.
Msemaji alisema: “Pamoja na washirika wetu, tunaongeza mwitikio wetu kwa ukamataji wa meli zilizokiuka vikwazo – na tutaendelea kufanya hivyo.”
