#HABARI: Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Korea zimefanya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Rufiji kama mpango wa muda mrefu wa kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa ambapo utatoa maji kwenye chanzo cha Mto Rufiji na kuyafikisha Dar es Salaam na maeneo jirani kwa ajili ya huduma ya maji.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mhe. Eun Ju Ahn kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo katika Sekta ya Maji kwa kutekleza miradi mbalimbali ya maji nchini.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dodoma, yalijikita katika masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, hususan katika maeneo ya kuimarisha huduma ya majisafi na majitaka, rasilimali za maji pamoja na usalama wa maji, uvunaji wa maji ya mvua pamoja na fursa mpya za uwekezaji katika Sekta ya Maji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania