Iran imewasilisha malalamiko rasmi kwa Umoja wa Mataifa kufuatia matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump, ikimkemea kwa kutoa vitisho vya kijeshi na kuwachochea waandamanaji kuteka taasisi za serikali.

Katika barua iliyomwendea Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Rais wa Baraza la Usalama Samuel Zbogar siku ya Jumanne, Balozi wa Iran na Mwakilishi wa Kudumu, Amir Saeid Iravani, aliashiria kauli ya Trump ambayo inachochea waziwazi vurugu ndani ya Iran na kutishia kuingilia kijeshi.

Trump alisema katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa kijamii kwamba: 

Akiwahutubu waandamanaji wa Kiirani, Trump alisema: “Wazalendo wa Iran, ENDELEENI KUANDAMANA—CHUKUENI TAASISI ZENU!!! … MSAADA UPO NJIANI.”

Iravani amesisitiza kuwa kauli hii ya kiholela “inachochea wale wanaotaka kuvuruga utulivu wa kisiasa, inawataka watu waibue ghasia na fuji, na inatishia mamlaka, umoja wa kitaifa na usalama wa taifa la Iran.”

Katika siku za karibuni, Trump na maafisa wengine wa Marekani walisema kuwa Marekani ingechukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran endapo kile walichokiita “kukandamiza” ghasia zilizotokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran, rial, kingeendelea.

Iravani amebainisha kuwa matamshi ya Trump ni ukiukaji wa wazi wa misingi ya sheria za kimataifa iliyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa, hususan marufuku ya kutishia au kutumia nguvu na kanuni ya kutokuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine.

Barua hiyo ilieleza kuwa matamshi ya Trump yanapaswa kuangaliwa katika muktadha wa kushindwa kwa vita vya siku 12 dhidi ya Iran mnamo Juni 2025, na kama sehemu ya sera pana ya kupindua utawala wa Kiislamu Iran inayojumuisha “shinikizo la juu kabisa,” vikwazo vya upande mmoja vilivyopanuliwa, juhudi za makusudi za kuvuruga jamii na uchumi, pamoja na kuchochea machafuko miongoni mwa vijana wa Iran.

Mnamo Juni 13, Israel ilianzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran, ambapo iliwaua makamanda waandamizi wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia na raia wa kawaida.

Zaidi ya wiki moja baadaye, Marekani nayo iliingia vitani kwa kushambulia maeneo matatu ya nyuklia ya Iran, hatua ambayo Iran imeitaja kuwa ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Katika kujibu, Vikosi vya Ulinzi vya Iran vililenga maeneo ya kimkakati katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) pamoja na kituo cha kijeshi cha al-Udeid nchini Qatar, ambacho ndicho kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika Asia ya Magharibi. Baada ya hapo Wazayuni na Wamarekani waliomba vita visitishwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *