Kamati Kuu ya ACT Wazalendo inatarajiwa kukutana Januari 18 mwaka huu na kisha kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ambavyo pamoja na mambo mengine vitatoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na ushiriki wa chama hicho kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 2025.
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Isihaka Mchinjita, ameeleza hali ya sintofahamu iliyoibuka kufuatia chama hicho kususia kushiriki kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar huku kukiwa wazi nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar na nafasi nne za Mawaziri baada ya chama hicho kuwa chama cha pili kwa idadi ya kura ilizopata wakati wa uchaguzi mkuu.
#StarTvUpdate