Chama cha ACT Wazalendo kimekanusha taarifa za kuwa kwenye msigano na aliyekuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita Luhaga Mpina ambae baadae alienguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kuwekewa pingamizi.

Taarifa inayojadiliwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii inaeleza kuwa Mpina aliyejiunga na chama hicho akitokea chama cha Mapinduzi (CCM) siku chache baada ya jina lake kukatwa kwenye orodha ya watia nia nafasi ya ubunge wa jimbo la Kisesa, yupo kwenye mvutano ama kutokuelewana na uongozi wa juu wa chama hicho kwa kile kinachoelezwa kwamba wapo baadhi ya viongozi wamehusika kwenye mchakato wa kuenguliwa kwake kugombea urais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita, ameeleza kuwa hakuna tofauti zozote zilizopo isipokuwa wapo watu wenye wivu na chama hicho wakiombea kiingie kwenye migogoro.

#StartvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *