Kampuni ya Azam Ice Cream imezindua rasmi bidhaa mpya ya ice cream yenye ubora wa hali ya juu, ikilenga kuwapatia wateja ladha mpya na chaguo pana kulingana na mahitaji yao.

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Meneja wa Oparesheni wa Azam Ice Cream, Hassan Shekh, amesema kwa sasa ice cream za Azam zinapatikana katika vifungashio bora na ujazo tofauti tofauti, hali inayowawezesha wateja kuchagua kulingana na matumizi yao, iwe ni ya mtu mmoja au kwa familia.

Ameeleza kuwa bidhaa hiyo imekuja na ladha mpya ambazo zimeandaliwa kwa kuzingatia vionjo vinavyopendwa zaidi na wateja.

Ice cream hiyo inapatikana katika ladha nne kuu, ambazo ni Vanilla, Vanilla Strawberry, Vanilla Chocolate na Strawberry, hivyo kumpa mteja uhuru wa kuchagua ladha inayokidhi matakwa yake.

✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *