Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi, amesema Serikali imeweka mkakati wa kitaifa wa kuongeza uzalishaji wa dawa za ndani ifikapo mwaka 2030, ili kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje.

Amesema kupitia mkakati huo, lengo ni kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2030, dawa zinazoagizwa kutoka nje zitapungua hadi chini ya asilimia 40, huku zaidi ya asilimia 60 zikitokana na viwanda vya ndani.

Kwa sasa, Tanzania huzalisha takribani asilimia 20 ya mahitaji ya dawa, hali ambayo imesababisha Serikali kuanza kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa viwanda vya dawa, ikiwemo kuwapatia nafasi kubwa katika masoko ya ndani ili kuongeza uzalishaji na kujenga uwezo wa nchi kujitegemea katika sekta ya dawa.

✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *