‎#HABARI: Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kigoma kuhakikisha anamsimamia kwa karibu mkandarasi anayejenga barabara ya Malagarasi–Ilunde–Uvinza kwa kiwango cha lami ili ikamilike kabla ya mwisho wa mwezi Februari mwaka huu.

‎Mhe. Kasekenya ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wenye urefu wa kilomita 51.1, ambapo alisisitiza umuhimu wa kasi na ubora katika ujenzi wa barabara hiyo.

‎Amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha mkoa wa Kigoma unakuwa kitovu cha biashara kutokana na nafasi yake ya kimkakati ya kupakana na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia na Burundi.

‎Naibu Waziri ameongeza kuwa miradi ya miundombinu kama hiyo ni chachu ya kukuza uchumi wa wananchi na kufungua fursa mpya za uwekezaji katika ukanda wa Magharibi mwa Tanzania.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *