Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amewaonya maadui dhidi ya kufanya makosa yoyote ya kimahesabu, akisisitiza kwamba vikosi vyake viko tayari kutekeleza maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.

Meja Jenerali Mohammad Pakpour, katika ujumbe alioutoa Alhamisi, alisema: “Tunawaonya maadui waovu, wakatili na wanaopinga ubinadamu, hasa Marekani na utawala bandia wenye ubaguzi wa rangi wa Kizayuni, kujifunza kutokana na uzoefu wa kihistoria na kile walichokipata katika vita vya siku 12 [mwezi Juni], ili kuepuka kufanya makosa ya kimahesabu.” Aliongeza kuwa iwapo watathubutu kufanya kosa lolote, watakabiliwa na hatima “ya uchungu zaidi na ya kuleta majuto makubwa.”

Alisisitiza kwamba vikosi vya IRGC vimeimarisha kwa uthabiti kuliko wakati wowote ule uwezo wa ulinzi wa taifa na usalama wa nchi dhidi ya uadui na vitendo vya uharibifu vinavyohusishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni.

Mwishoni mwa Desemba, Iran ilishuhudia maandamano ya hapa na pale ya kiuchumi ambayo yalitekwa haraka na wahuni waliotiwa moyo na watawala wa Marekani na Israel, wakisaidiwa na mawakala wao wa kijasusi waliokuwapo nchini. Rais wa Marekani, Donald Trump, alihamasisha waziwazi matumizi ya vurugu kwa kuwataka wahuni wenye silaha kuchukua taasisi za serikali na kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran iwapo wangekabiliwa. Katika makala ya maoni iliyochapishwa na The Wall Street Journal siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi alisema vitisho vya Trump dhidi ya Iran vilikuwa kichocheo cha moja kwa moja kwa seli za kigaidi kufuata mkakati wa “umwagaji damu wa kiwango cha juu” ili kuivuta Marekani kuingia katika vita vingine kwa niaba ya Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *