#HABARI: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mheshimiwa John Heche, amefika msibani kwa marehemu Mzee Edwin Mtei katika eneo la Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
Mheshimiwa Heche amesema msiba huo ni wa wanachama wote wa CHADEMA na kutoa pole za dhati kwa familia ya marehemu huku pia akikutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Ameeleza kuwa chama kiko pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu na kitahakikisha Mzee Mtei anazikwa salama na kupewa heshima yake stahiki kama mmoja wa waasisi wa chama.

(Feed generated with FetchRSS)