London. Tottenham Hotspur na Liverpool zipo kwenye majadiliano ya kuuziana beki Andy Robertson kwa dau la Pauni 5 milioni (Sh17 bilioni).

Nahodha huyo wa Scotland mkataba wake na Liverpool utafikia tamati mara baada ya msimu huu kumalizika na alikuwa katika hesabu za usajili za Spurs kwa muda mrefu.

Hata hivyo uwepo wa wachezaji kadhaa majeruhi na uhitaji wa mchezaji kiongozi katika chumba cha kubadilishia nguo, umefanya Spurs kuweka nguvu katika usajili wa Robertson.

Mazungumzo ya awali baina ya Liverpool na Spurs yameshafanyika juu ya uhamisho wa Robertson na yanategemewa kukamilika siku chache zijazo.

Beki huyo leo atakuwa na kikosi cha Spurs ambacho kinakabiliwa na mchezo wa ugenini dhidi ya Bournemouth.

Robertson mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea Hull City kwa Pauni8 milioni (Sh28 milioni).

Tangu hapo hadi sasa amejitambulisha kama miongoni mwa wachezaji ambao usajili wao umefanikiwa zaidi ya thamani aliyonunuliwa.

Beki huyo ameshaichezea Liverpool idadi ya michezo 363 katika mashindano yote tangu aliposajiliwa na ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu England huku akichukua Taji moja la Ligi ya Mabigwa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *