Tovuti ya habari ya Axios imeripoti kuwa Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Vladimir Zelensky wanaweza kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana muda si mrefu ujao ikiwa mazungumzo yanayoendelea kati ya nchi zao na Marekani yataendelea kufanyika.

Mazungumzo ya amani baina ya pande tatu yaliyofanyika huko Abu Dhabi kwa muda wa siku mbili na kumalizika Jumamosi, yalikuwa ya kwanza kuwakutanisha pamoja wajumbe wa Russia, Marekani na Ukraine tangu mzozo kati ya Moscow na Kiev ulipopamba moto karibu miaka minne iliyopita.

Siku ya Jumamosi, Axios ilimnukuu afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutajwa jina lake akisema, mazungumzo yaliyofanyika katika Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) “yalienda vizuri kama tulivyotarajia. Tunajisikia vizuri kwa tulipo hivi sasa”.

“Tuko karibu sana na mkutano kati ya Putin na Zelensky,” alidai afisa mwingine wa Marekani.

Mazungumzo zaidi baina ya pande tatu za Russia, Marekani na Ukraine “yanahitaji kujiri kabla ya mkutano kati ya viongozi. Hatudhani kama tuko mbali na hilo. Tukiendelea na njia ya sasa tutafika mahali hapo,” kimeeleza chanzo hicho.

Afisa huyo wa Washington ameendelea kueleza kwamba, inayofuata ya mazungumzo ya pande tatu, iliyopangwa kufanyika Februari Mosi huko Abu Dhabi, inaweza kufungua mlango wa mkutano utakaofanyika huko Moscow au Kiev.

Putin na Zelensky walikutana ana kwa ana mara ya mwisho huko mjini Paris, Ufaransa mnamo Desemba 2019 wakati wa mazungumzo yaliyosimamiwa na Ufaransa na Ujerumani. Wawaili hao walizungumza kwa simu mara mbili mwaka uliofuata…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *