#HABARI: Zaidi ya wananchi 1,000 mkoani Manyara wameanza kunufaika na Kambi Maalum ya Matibabu inayotolewa na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
Kambi hiyo inalenga kutoa huduma za kibingwa katika magonjwa ya mifupa, koo, macho, pamoja na kufanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa wenye mahitaji hayo.
Wananchi waliopata matibabu, akiwemo Emmanuel Julius na Amina Mndeme, wameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma hizo karibu, wakieleza kuwa kambi hiyo imewapunguzia gharama na usumbufu wa kufuata huduma za kibingwa mikoa ya mbali.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Manyara, Dkt. Yesige Mutajwa, amesema wanatarajia kuhudumia idadi kubwa ya watu ili kukabiliana na changamoto za kiafya mkoani humo.
Aidha, wadau wa afya walioshiriki katika kambi hiyo wamepongeza ushirikiano uliopo kati ya hospitali hizo mbili, wakisisitiza kuwa kambi kama hizi ni muhimu katika kuimarisha ustawi wa jamii.
Jitihada hizi ni sehemu ya mikakati ya kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha huduma bora za matibabu zinawafikia wananchi wote bila kujali kipato au mahali walipo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.