#HABARI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, imeendelea kuwajengea uwezo wafanyabiashara pamoja na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwa kutoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo mpya wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS).
Mafunzo hayo yamelenga kuboresha utoaji wa huduma za kikodi, kuongeza ufanisi katika ulipaji na ukusanyaji wa kodi, pamoja na kurahisisha usimamizi wa masuala ya kikodi kwa walipakodi nchini.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. James Jilala, amesema kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa IDRAS kutarahisisha kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa kodi, kupunguza usumbufu kwa walipakodi, na kuongeza uwazi katika mifumo ya kifedha.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, ameeleza kuwa mfumo huo pia utachochea ukuaji wa uchumi kwa kuwezesha wafanyabiashara kutekeleza wajibu wao wa kikodi kwa urahisi na kwa wakati, hivyo kuongeza mapato ya serikali kwa maendeleo ya taifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.