Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kuunga mkono jitihada za taasisi na sekta binafsi zinazolenga kuinua wabunifu na wajasiriamali, ili kuwawezesha kujiajiri na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Harun Makandi wakati akizungumza katika programu ya Funguo, inayotekelezwa kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), yenye lengo la kuwawezesha wajasiriamali kutoka vyuo vikuu.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John MBalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *