‎#HABARI: Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi John Mongela amesema ameridhika na hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo cha Afya cha Tinde, wilayani Shinyanga, huku akieleza kuchukua changamoto ya upungufu wa majengo ya kutolea huduma ya upungufu wa wahudumu wa afya kuzifanyia kazi.

Naibu Katibu Mkuu John Mongela ameyasema hayo baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho cha afya Tindr pamoja na kuwapatia mahitaji ya kibinadamu.

Nao wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo wamesema wameridhika na huduma wanazopatiwa huku wakiomba ziboreshwe zaidi ili kukidhi mahitaji ya huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo.

Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya Dkt. Evance Munisi amesema kituo hicho kinahudumia wananchi wengi kwakuwa kipo njiapanda ya Barabara ya Tabora Shinyanga na Shinyanga Kahama ambapo ameomba Serikali ione kuwa kuna haja ya kuongeza miundombonu wezeshi.‎

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *