‎#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewaagiza wakulima mkoani humo kuacha kususia kilimo cha alizeti na badala yake kila mmoja alime angalau hekari mbili ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula nchini.

Akizungumza wilayani Ikungi wakati wa kuhitimisha kampeni ya kitaifa ya upandaji miti ya BAKWATA, Mkuu wa Mkoa alibainisha kuwa kasi ya uzalishaji wa zao hilo la kimkakati imepungua kwani wakulima wengi wameelekeza nguvu zao kwenye kilimo cha mahindi pekee.

Katika hafla hiyo, Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Omary Muna, alieleza mafanikio ya kampeni hiyo ya mazingira iliyozinduliwa na Mufti Abubakar Zubeir, ambapo hadi sasa miti milioni 1.4 imepandwa katika wilaya 52 nchini tangu mwaka 2024.

Hata hivyo, baadhi ya wakulima wa kijiji cha Mnang’ana walipata nafasi ya kueleza changamoto zinazowafanya wasichelee kulima alizeti, huku wakitakiwa kuongeza juhudi ili kufikia malengo ya kimkakati ya mkoa na taifa.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *