#HABARI: Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka mkandarasi wa kampuni ya CCC International Engineering kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 135 mkoani Ruvuma baada ya kusuasua kwa utekelezaji wake.
Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya REA, Mha. Deogratius Nagu, ameeleza kuwa hadi sasa mkandarasi amefikia asilimia 56 pekee badala ya asilimia 80 inayotakiwa, huku akiwasha vitongoji 43 tu kati ya vyote vilivyopangwa.
Ili kukamilisha mradi huo wa shilingi bilioni 14.56 kwa wakati, REA imemuelekeza mkandarasi kumbadilisha Meneja wa Mradi, kuongeza timu za mafundi, na kuhakikisha vifaa kama transfoma na nyaya vinapatikana kwa haraka.
Ingawa mkandarasi amekiri kuchelewa kutokana na changamoto za upatikanaji wa vifaa, ameahidi kutekeleza maelekezo hayo ili kuwafikishia huduma wateja zaidi ya 5,400 ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.