Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kitaendelea kuhakikisha kinaisimamia Serikali yake katika kuboresha na kulinda maslahi ya wafanyakazi wote Nchini Ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

Kuelekea maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha mapinduzi CCM, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdalah akiongozana naKamati ya siasa ya Mkoa, wamefanya ziara ya kutembelea katika hospital ya Wilaya ya Lushoto kwa lengo la kujionea hali ya kiutendaji, kuwafariji na kuwashika Mkono Wagonjwa waliolazwa katika hospital hiyo

Baada ya ziara ya hospitali, viongozi hao walifanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Wilaya hiyo, ambapo walitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi Ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za mwanzo Wananchi wapate Bima za Afya.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilianzishwa rasmi Februari 5, mwaka 1977

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *