Chanzo cha picha, Armed Forces of Ukraine/Telegram
Ndege isiyo
na rubani inayomilikiwa na Urusi, ilishambulia basi moja ambalo lilikuwa limewabeba
wafanyikazi wa migodini mashariki ya kati ya eneo la Dnipropetrovsk.
Shambulio
hilo la hapo jana liliwauwa watu 12 waliokuwa kwenye basi hilo lililokuwa
karibu na maeneo ya Ternivka, mji ulioko kilomita 65, kutoka enela vita,
kulingana na polisi wa eneo hilo.
Kampuni ya
nishati ya DTEK nchini Ukraine, imesema wale waliouawa walikuwa wafanyikazi wa
kampuni hiyo, ambao walikuwa wamemaliza zamu yao ya kazi.
Shambulio
hilo lilitokea wakati ambapo kumekuwa na makubaliano ya kupunguza mashambulizi
ya Urusi dhidi ya Ukraine.
Rais wa
Marekani Donald Trump alikuwa ametangaza kuwa vita hivyo viko karibu
kumalizika, na kuongezea kuwa Rais Putin wa Urusi alikuwa amekubali kusitisha
mashambulizi kutokana na hali ya baridi inayoshuhudiwa kwa sasa.
Mapema
Jumapili, ndege isiyo na rubani ilishambulia hospitali moja ya kujifungua kina
mama eneo la Zaporizhzhia, na kuwajeruhi wanawake saba waliokuwa wakipokea
matibabu.
Soma zaidi: