#HABARI: Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, amewahakikishia wakulima nchini kuwa Wizara ya Kilimo itaendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa miradi yote iliyoahidiwa na Serikali, ikiwemo miradi ya umwagiliaji, ujenzi wa masoko ya mazao, na utoaji wa ruzuku za pembejeo za kilimo, kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Silinde ameeleza haya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, na kwamba Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha changamoto zinazowakabili wakulima zinapatiwa suluhisho la kudumu.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha sekta ya Kilimo inabaki kuwa nguzo ya uchumi wa taifa, ikileta tija kwa wakulima wadogo na wa kati nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.