#HABARI: Vijana kutoka makundi mawili mkoani Mwanza, waliowasilisha mawazo yao kupitia Wizara ya Vijana mnamo Januari mwaka huu, wamepatiwa jumla ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi yao ya maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, kila kundi litapokea shilingi milioni 100, ambapo kundi la kwanza ni Kitwima Youth Group, huku kundi la pili likiwa ni Waendesha Bajaji za Mizigo na Pickup.
Fedha hizo zinalenga kuwawezesha vijana hao kukuza shughuli zao za kiuchumi, kuongeza ajira pamoja na kuhamasisha ubunifu na ushiriki wa vijana katika maendeleo ya jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.