Ingawa Israel na Marekani zimeonya kwamba Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, aliyeteuliwa siku ya Jumapili jioni, atalengwa na mashambulizi, China imesema leo Jumatatu kwamba inapinga hatua yoyote ya nchi ya kigeni inayomlenga Kiongozi huyo mkuu wa Iran.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

China imesema Jumatatu kwamba inapinga hatua yoyote ya nchi ya kigeni inayomlenga Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei. “China inapinga kuingiliwa kwa mambo yoyote ya ndani ya nchi nyingine, kwa kisingizio chochote kile, na uhuru, usalama, na uadilifu wa eneo la Iran lazima uheshimiwe,” amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari, alipoulizwa kuhusu vitisho vya Marekani na Israel.

Israel ilionya Jumatano kwamba Kiongozi Mkuu mpya wa Iran “atalengwa” na mashambulizi,” hata kabla ya uteuzi wa Mojtaba Khamenei. Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba Kiongozi Mkuu mpya “hautadumu kwa muda mrefu” bila idhini yake.

Hasira ya China kuhusu operesheni za kijeshi za Marekani na Israel

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amewasilisha uteuzi wa Mojtaba Khamenei kama jambo la ndani la Iran. “Tumezingatia taarifa kuhusu jambo hili. Huu ni uamuzi uliofanywa na upande wa Iran kwa mujibu wa Katiba yake,” amesema.

Beijing imeonyesha hasira yake kuhusu operesheni za kijeshi za Marekani na Israel na kifo cha Kiongozi Mkuu wa zamani, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuawa siku ya kwanza ya vita na ambaye Mojtaba Khamenei anamrithi. “China inatoa wito kwa (pande husika) kusitisha shughuli za kijeshi mara moja, kuanzisha tena mazungumzo haraka iwezekanavyo, na kuepuka kuongezeka kwa mvutano,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya NJe amebainisha. Zaidi ya 80% ya mauzo ya nje ya mafuta ya Iran yalikwenda China kabla ya vita, kulingana na kampuni ya uchambuzi ya Kpler.

Mafuta ya Iran yalitarajiwa kuchangia 13% ya uagizaji wa mafuta ya China ifikapo mwaka wa 2025, kulingana na Kpler. China imeathiriwa moja kwa moja na kizuizi cha Mlango Bahari wa Hormuz: zaidi ya nusu ya uagizaji wake wa mafuta ghafi ya baharini hutoka Mashariki ya Kati na hupitia hasa kwenye mlango bahari, kulingana na Kpler.

Ziara ya Trump nchini China imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Machi

Hata hivyo, wataalamu wanaona kuwa haiwezekani kwamba China itatoa itajitolea maslahi yake na kusimama mbele ya Marekani ili kumsaidia mshirika wake wa Iran, hasa wiki chache tu kabla ya ziara inayowezekana ya Rais Trump nchini China mwishoni mwa mwezi Machi au mapema mwezi Aprili.

Beijing imekuwa ikifanya kazi katika upande wa kidiplomasia. Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi amezungumza na wenzake kadhaa katika siku za hivi karibuni. Beijing imemteua mjumbe wa upatanishi. Mjumbe huyu, Zhai Jun, alikutanasiku ya Jumapili na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza leo Jumatatu. Pia amekutana na Jasem al-Budaiwi, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC), kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *