Nchini kenya idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa wiki iliopita, imeongezeka kutoka 23 na sasa idadi hiyo imefikia watu 45, kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mbali na idadi ya vifo kuongezeka, idara ya polisi nchini humo imesema waru wapatao 2224 pia walilazimika kuyahama makazi yao, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.
Mvua kubwa zilizoshuhudiwa Ijumaa iliopita katika jiji kuu la Niarobi lilisababisha barabara za mji huo kufurika huku maelfu ya nyumb na biashara pia zikiathirika na mafuriko hayo.
Siku ya Jumamosi, mamlaka za polisi zilitangaza kuwa idadi ya watu waliokuwa wamefariki ilikuwa 23, lakini ikasema inaendeleza shughuli za utafutaji na uokoaji.
Tangu kutokea kwa mafuriko hayo, wenyeji wa mji huo wamekuwa wakielezea ghadhabu yao kwa gavana wa jmbo hilo Johnson Sakaja ambaye alipochukuwa madaraka 2022, aliahidi kuboresha mifumo ya mabomba ya kupitisha majitaka pamoj ana barabara za mji huo.
Ndani ya miaka 20 iliopita, tafita kadhaa zimekuwa zikifuatilia kuongzeka kwa matukio ya mismu ya baridi na ukame kupita kiasi katika eneo la Afrika Mashariki, wanasayansi wakionya kuhusu hali ya mabadiliko ya tabianchi inayosababishwa na binadamu.
