Niger: Milio ya risasi yasikika karibu na uwanja wa ndege wa TahouaNiger: Milio ya risasi yasikika karibu na uwanja wa ndege wa Tahoua

Nchini Niger, usiku wa kuamkia Jumatatu milio mizito ya silaha za kivita imesikika karibu na uwanja wa ndege wa Tahoua na kuzua hali ya wasiwasi kwa raia wanaoishi karibu na uwanja huo wa ndege.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo ya risasi yalidumu kwa takriban dakika 30, kabla ya hali ya utulivu kurejea, lakini hali hiyo imeacha hali ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wanaoishi karibu na uwanja huo wa ndege.

Ripoti zaidi zinasema, watu waliokuwa wamejihami kwa silaha wakiwa kwenye pikipiki walijaribu kuuvamia uwanja huo, lakini wakakabiliwa vikali na maafisa wa usalama wa Niger.

Uwanja wa ndege wa Tahoua, upo kwenye eneo la mkakati nchini Niger ambao kwa muda mrefu umekuwa katika hali ya hatari kwa sababu za kiusalama, unapakana na nchi za Mali na Nigeria, nchi ambazo zimeendelea kusumbuliwa na makundi ya kijihadi.

Hii ni mara ya pili kwa uwanja wa ndege wa Niger, kulengwa na watu wenye silaha, baada ya jaribio lingine kama hili, kushuhudiwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Diori Hamani, jijini Niamey Januari 27 mwaka huu, usiku wa kuamkia tarehe 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *