Serikali kupitia Waziri wa fedha Balozi Khamis Mussa Omar, imesema itafanya mageuzi makubwa ya uchumi ikiwemo mfumo wa uzalishaj…Serikali kupitia Waziri wa fedha Balozi Khamis Mussa Omar, imesema itafanya mageuzi makubwa ya uchumi ikiwemo mfumo wa uzalishaj…

Serikali kupitia Waziri wa fedha Balozi Khamis Mussa Omar, imesema itafanya mageuzi makubwa ya uchumi ikiwemo mfumo wa uzalishaji wa viwanda na kuifungua nchi kwa miundombinu itakayosaidia kuleta maendeleo ya haraka kupitia miradi ya PPP.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri waziri wa fedha Balozi Khamis Mussa Omar, wakati akifungua mafunzo ya 17 ya kozi fupi kwa watendaji na viongozi waandamizi wa serikali na sekta binafsi ambapo katika hotuba yake ya ufunguzi amesema sekta binafsi inapaswa kupewa nafasi kama mbia muhimu wa maendeleo.

Waziri huyo wa fedha ametoa wito kwa watoa mada na washiriki kutafuta majawabu juu ya changamoto zinazokwamisha miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yaani PPP kutofanya vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania Meja Jenerali Wilbert Ibuge amesema chuo hicho kimeandaa mafunzo hayo kwa kutambua umuhimu wa watendaji na watoa maamuzi kuwa na mawazo yanayounganika.

Kozi fupi ya 17 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania itafanyika kwa siku tano ikihusisha washiriki 100 ambao miongoni mwao ni makatibu tawala wa mikoa, watendaji wakuu wa taasisi za umma, maafisa wakuu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama taasisi za fedha na watendaji wakuu waandamizi kutoka sekta binafsi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *