
Maelfu ya wananchi wa Sudan Kusini waliokimbilia katika ngome ya upinzani katika Mji wa Akobo, unaopakana na Ethiopia, Mashariki mwa nchi hiyo, wameagizwa kuondoka katika eneo hilo kufikia leo, wakati huu wanajeshi wa serikali wanapojiandaa kuvikabili vikosi vya upinzani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita mji huo ulianza kusalia bila watu, baada ya agizo hilo la jeshi Ijumaa iliyopita.
Mbali na raia wa kawaida, wafanyakazi kutoka mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, nao pia wametakiwa kuondoka.
Nhial Lew, mmoja wa kiongozi wa shirika la kiraia katika mji wa Akobo amesema, wanawake, watoto na wazee wameondoka na kukimbilia nchi jirani ya Ethiopia.
Aidha, ameeleza kuwa kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, milio ya zana za kivita, zimeanza kusikika.
Mji wa Akobo umekuwa kimbilio la maelfu ya wakimbizi wapatao 82,000 na imekuwa ngome ya kiongozi wa vikosi vya upinzani SPLM-IO, Riek Machar ambayo vimekuwa vikipambana na vile vya serikali tangu mwaka 2025.
