DNA yamkataa aliyedai ni mama mzazi wa msanii BahatiDNA yamkataa aliyedai ni mama mzazi wa msanii Bahati

Kenya. Miezi michache iliyopita mwanamke mmoja ambaye jina lake halijawekwa wazi alizua gumzo katika mitandao ya kijamii akidai, yeye ndiyo mama mzazi wa mwanamuziki wa Kenya, Kevin Bahati. 

Kauli hiyo iliwashangaza wengi, akiwemo Bahati mwenyewe. Kwani anachokifahamu yeye ni kuwa mama yake alifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka saba.

Hatahivyo baada ya madai hayo kuibuka, mwanamke huyo aliendelea kusisitiza kuwa Bahati ni mwanae wa kumzaa. Alieleza miaka iliyopita alimuacha mtoto wake katika kituo cha kulea watoto yatima kwa muda, lakini aliporudi kumchukua alimkosa.

Tangu wakati huo aliamini huenda mtoto huyo alichukuliwa na familia nyingine. Jambo linalomfanya kuhisi Bahati ndiye mtoto wake.

Kwa upande wake, Bahati hakukubaliana na madai hayo kwa muda mrefu alionekana kumkwepa mwanamke huyo. Huku akisisitiza kuwa anamfahamu mama yake na historia ya maisha yake ya utotoni. 

Aidha, kutokana na msisitizo wa mwanamke huyo na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Bahati alikubali kufanya kipimo cha DNA na mama huyo ili kubaini ukweli.

Baada ya kipimo kufanyika mapema mwishoni mwa Februari. Majibu yametoka jana Machi9,2026 yakiweka wazi hakuna uhusiano wa damu kati ya wawili hao. Matokeo yanaonesha kuwa kiwango cha mfanano wao ni asilimia 0, jambo linalothibitisha kuwa mwanamke huyo si mama mzazi wa Bahati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *