Kenya: Shirila la mafuta KPC laorodheshwa katika soko la hisa la NairobiKenya: Shirila la mafuta KPC laorodheshwa katika soko la hisa la Nairobi

Rais wa Kenya, William Ruto, ameongoza hafla maalumu ya kuliorodhesha shirika la mafuta la nchi hiyo KPC katika soko la hisa la Nairobi, hatua inayolenga kuvutia uwekezaji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto amesema kupitia ubinafsishaji walioufanya, shirika hilo limefanikisha kupatikana kwa shilingi za Kenya Bilioni 106 kutoka Bilioni 5 walizokuwa wakipata kama faida miaka iliyopita, ambapo ameongeza kuwa fedha hizo kupitia mfuko wa kitaifa wa miundombinu utasababisha nchi kupata shilingi za Kenya trilioni 1.2 kwa ajili ya kufadhili miradi ya ndani ya maendeleo.

Hatua ya kuliorodhesha shirika hili inamaanisha kuwa sasa wakenya wa kawaida, wafanyabishara wawekezaji wa ndani na nje, wataweza kununua hisa za shirika hilo.

Wakenya wa kawaida, wafanyabishara wawekezaji wa ndani na nje, sasa wanaweza kununua hisa za shirika hilo.
Wakenya wa kawaida, wafanyabishara wawekezaji wa ndani na nje, sasa wanaweza kununua hisa za shirika hilo. © Ikulu ya Nairobi

Tangu aingie madarakani, rais William Ruto amekuwa akipigia chapuo mpango wa serikali yake kubinafsisha baadhi ya mashirika ya uma aliyosema yalikuwa yanatengeneza hasara, mpango ambao hata hivyo tangu mwaka 2023 umekutana na vikwazo vya kisheria.

Mpaka sasa serikali yake imeruhusu ubinafsishwaji wa mashirika zaidi ya 11, ikiwemo kituo cha kimataifa cha mikutano cha KICC na shirika la mbegu la taifa, hata hivyo mwaka jana mahakama iliagiza mkakati huo kusitishwa kwa kile ilidai hakukuwa na ushirikishwaji wa uma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *