M23 inapanga kuwaachia huru wafungwa wa kijeshi wa serikaliM23 inapanga kuwaachia huru wafungwa wa kijeshi wa serikali

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waasi wa AFC/M23, wanasema wana mpango wa kuwaachia huru mamia ya wafungwa wa kijeshi wa serikali, wanaoshikiliwa katika maeneo wanayodhibiti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa waasi hao unasema unapanga kuwakabishi wanajeshu hao wa FARDC kwa Shirika la Kimataifa la Masalaba Mwekundu, kwa mujibu wa makubaliano ya Doha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa RFI wanajeshi wa FARDC wapatao 2,700, wanatarajiwa kuachiwa huru, lakini Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, halijathibitisha idadi hiyo.

Hata hivyo, Shirika hilo limesema, limepokea taarifa ya kuwepo kwa mpango huo ambao M23/AFC wanasema, unaonesha nia njema ya kupata mwafaka wa mzozo Mashariki mwa DRC.

Kwa upande mwingine, serikali jijini Kinshasa inasema, haijapokea taarifa yoyote kutoka kwa waasi hao, na kudai kuwa kinachofanyika ni kundi hilo kutafuta umaarufu wa kisiasa na huruma ya  kidiplomasia.

Mwezi Septemba mwaka 2025 waasi hao na serikali ya DRC walitia saini makubaliano ya kuwachiwa kwa wafungwa wote, laini mpaka sasa hakuna aliyewahi kuachiwa huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *