Madagascar : Kiongozi wa kijeshi amfuta kazi Waziri wake MkuuMadagascar : Kiongozi wa kijeshi amfuta kazi Waziri wake Mkuu

Kiongozi wa kijeshi nchini Madagascar Kanali Michael Randrianirina, amemfuta kazi Waziri Mkuu wake na kulivunja baraza lake la Mawaziri, aliloteua baada ya kuchukua madaraka miezi mitano iliyopita, baada ya maandamano ya vijana.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Randrianirina kupitia msemaji wake amesema, serikali imevunjwa mara moja na Waziri Mkuu Herintsalama Rajaonarivelo, ameondolewa kwenye nafasi hiyo.

Aidha, kiongozi huyo wa Madagascar ambaye hakueleza ni kwanini ameivunja serikali amesema, Waziri Mkuu mpya atateuliwa hivi karibuni.

Randrianirina, alichukua hatamu za uongozi baada ya maandamano yaliyoanza mwezi Septemba mwaka uliopita, kulalamikia uhaba wa maji na umeme, kusababisha kuangua kwa utawala wa rais wa wakati huo Andry Rajoelina, aliyekimbia nchi.

Baada ya kuchukua madaraka, Kanali huyo, alikanusha madai kuwa, alichukua mamlaka kwa nguvu na badala yake kudai kuwa alikabidhiwa na Mahakama ya Katiba, ambapo ameahidi kuongoza kwa kipindi cha mpito cha miaka miwili  na kuahidi katiba mpya na uchaguzi wa urais mapema mwaka 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *