
Miaka minne imepita tangu vyama vya michezo duniani vichukue hatua ya kuifungua Urusi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine, hata hivyo uvamizi wa Marekani na Israel kwa nchik ya Iran ukiibua maswali ya upendeleo kwa vyama hivyo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vita zote hizi zilizuka baada ya kumalizika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na kabla ya michezo ya watu wenye ulemavu na kuelekea michuano ya kombe la dunia ya wakati wa majira ya joto.
Urusi ilivamia Ukraine siku nne baada ya sherehe za kufungwa kwa michuano ya Beijing mwaka 2022.
Marekani na Israel zilianza kuishambulia Iran siku 6 baada kumalizika kwa michezo ya Olimpiki majira ya baridi huko Milan-Cortina nchini Italia.
Mwaka 2022, ilichukua siku 4 tu kwa shirikisho la soka duniani FIFA na lile la Ulaya UEFA wakiungwa mkono na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, kuwafungia wanamichezo wa Urusi na Belarus.
IOC ililaani “ukiukwaji wa makubaliano ya Olimpiki na serikali ya Urusi na Belarusi ambayo iliiunga mkono Moscow kwenye vita ya Ukraine.”
Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wametathmini namna Urusi ilifungiwa na FIFA katika mashindano yake kufuatia uvamizi wake huko Ukraine, licha ya kuwa hakukuwa na majadiliano yaliyofanywa kama ambavyo yanafanyika na Marekani ambayo itakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu.
Wakosoaji wanahoji kwanini mpaka sasa vyama vya michezo duniani havijaichukulia hatua Marekani na Israel kutokana na uvamizi wao huko Iran.
Kwa baadhi wanaona kuwa FIFA, UEFA na IOC zinaiogopa Marekani ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za dunia, na hasa namna ilivyojitwika kwa uzuri jukumu la maandalizi ya fainali za kombe la dunia mwaka 2026.
Aidha urafiki wa rais Donald Trump na rais wa Fifa Gianni Infantino, ukiongeza muktadha wa kwanini shirikisho hilo limeshindwa kuchukua hatua, baadhi ya wakosoaji wakitaka Marekani kunayang’anywa uenyeji.
