Wachezaji 5 wa timu ya Iran wapewa hifadhi na AustraliaWachezaji 5 wa timu ya Iran wapewa hifadhi na Australia

Wachezaji watano wa timu ya taifa ya wanawake ya Iran ya mpira wa miguu, wamepewa hifadhi ya ukimbizi na mamlaka za Australia, wakiomba ulinzi baada ya kutajwa kama ‘wasaliti’ nyumbani kwao kwa kukataa kuimba wimbo wa taifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa Iran walikaa kimya wakati wimbo wa taifa lao ukipigwa katika mashindano ya kombe la mataifa ya ukanda wa Asia wiki iliyopita, kitendo ambacho kilitafsiria kama kuonesha Kwenda kinyume na utawala wa kiislamu wa Tehran.

Rais wa Marekani, Donald Trump, alikuwa miongoni mwa watu walioiomba Australia kutoa hifadhi kwa wachezaji hao, akihofia usalama wao ikiwa wangelazimishwa kupanda ndege kurejea nyumbani.

Wachezaji watano, akiwamo nahodha Zahra Ghanbari, walitoroka katika hoteli waliyofikia usiku wa manane na kuùba msaada toka kwa maofisa wa serikali ya Australia.

Waziri mkuu wa Australia, Anthony Albanese amesema “tumekuwa tikijiandaa kwa hili muda mrefu kidogo.”

“Raia wa Australia wamekuwa wakiguswa na ujasiri wa wasichana hawa. Wako salama hapa na wanapaswa kujisikia wako nyumbani”, alisema Albanese.

Waziri mkuu Albanese alivishukuru vyombo vya Habari kwa kufanya tukio hili kuwa siri, hadi pale wachezaji hawa walipokuwa salama.

Waziri wa mambo ya ndani wa Australia, Tony Burke, amesema serikali yake ilitumia siku kadhaa kwa usiri mkubwa kuzungumza na wachezaji hao, ambao baadae walichukuliwa hadi katika makazi salama baada ya kuondoka kwenye hoteli yao huko Gold Coast.

Picha zimewaonesha wachezaji hao wakiwa katika meza moja wakitia Saini nyaraka zilizowafanya wapewe viza maalum za kukaa Australia chini ya misingi ya kibinadamu.

Waziri Burke amesema wachezaji wengine wa Iran wanaruhusiwa kuomba hifadhi ya kubaki nchinik humo ikiwa watataka kufanya hivyo.

Hadi sasa haijabainika wazi ikiwa wachezaji waliosalia watasafiri Kwenda nyumbani au ni lini haswa wataondoka Australia.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na wanasiasa wa Iran wanaoishi nje ya nchi yao, walitoa wito kwa Serikali ya Canberra kutoa hifadhi kwa wachezaji hao kutokana na hofu kuwa ikiwa wangereja wangefanyiwa vitendo vya unyanyasaji, kwakuwa tayari walionekana kama wasaliti kwa nchi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *