
Wanajihadi wanaoshirikiana na magaidi Al-Qaeda wamewauwa watu 38 na kuwateka wanawake tisa nchini Burkina Faso kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch, linasema wanajihadi hao waliwauwa watu hao kati ya Januari 29 hadi Februari 22, katika matukio matatu tofauti nchini Burkina Faso.
Mashuhuda 10 wakiwemo wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wameshuhudua mauaji na mateso ya raia wa kawaida, mikononi mwa wanajihadi hao.
Januari tarehe 29, wanajihadi wa JNIM waliwateka wanawake tisa Kaskazini mwa kijiji cha Solle, wakitishia kuwabaka na kuwauwa, kabla ya kuwaachia huru siku iliyofuata.
Makundi ya kijihadi yameendelea kutatiza usalama wa Burkina Faso katika miaka ya hivi karibuni pamoja na eneo la Sahel, pamoja na nchi jirani kama Benin.
Jeshi lilichukua madaraka mwaka 2022 na kuahidi kumaliza wanajihadi nchini humo, lakini mpaka sasa hilo halijafanyika.