Licha ya kuwa mshirika wa kiitikadi wa Donald Trump barani Ulaya, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni haogopi kukemea kupuuzwa kwa sheria za kimataifa katika mashambulizi dhidi ya Iran, anaripoti mwandishi wetu huko Roma, Eric Senanque. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mabadiliko haya ya msimamo yanakuja huku Roma ikitangaza kurejeshwa kwa muda kwa wanajeshi 300 kutoka Kurdistan ya Iraq, waliolengwa Erbil kwa shambulio la ndege isiyo na rubani.

Siku ya Jumatano, Machi 11, mbele ya Bunge, Giorgia Meloni alikosoa vikali mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran, akilalamika kuhusu mwelekeo unaoongezeka wa kuingilia kati “nje ya mfumo wa sheria za kimataifa.” Vifo vya wasichana 168 wa Iran katika shambulio la kombora lililohusishwa na Marekani pia vimewaghadhabisha sana Waitaliano, na Waziri Mkuu alishutumu “mauaji” hayo. “Kwa sasa, Marekani haijaomba Italia ruhusa ya kutumia kambi mbalimbali za Marekani kwenye rasi hiyo kufanya mashambulizi yake nchini Iran, lakini Roma itahitaji kuidhinisha hili kupitia kura ya bunge. “Italia haiko vitani,” Giorgia Meloni alibainisha tena siku iliyotangulia, akifahamu kwamba maoni ya umma ya Italia yanabaki kuwa ya amani kwa kiasi kikubwa na ndio yanapewa nafasi katika maaamuzi ya hali kama hizo. Roma pia inataka mzozo huo kudumu kwa muda mfupi iwezekanavyo, kutokana na utegemezi wake mkubwa kwa gesi kutoka Ghuba.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *