Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema siku ya Alhamisi “ameshtushwa” na ripoti kwamba zaidi ya raia 200 wameuawa kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani nchini Sudan tangu Machi 4.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

“Inasikitisha sana kwamba, licha ya tahadhari kadhaa, maonyo, na wito, pande zinazohusika katika mzozo nchini Sudan zinaendelea kutumia ndege zisizo na rubani zenye nguvu zaidi kupeleka vifaa vya kulipuka vyenye athari kubwa kwa maeneo yenye watu,” Turk amesema katika taarifa.

Makumi ya raia wameuawa kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kusini mwa Sudan katika siku mbili zilizopita, vyanzo vya hospitali vililiambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano, kwani eneo hilo ndilo eneo linalokumbwa na mapigano makali zaidi katika vita vya karibu miaka mitatu.

Sudan imetumbukizwa katika mzozo tangu mwezi Aprili 2023, wakati mzozo wa kuwania madaraka kati ya jeshi la serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ulipoitumbukiza nchi hiyo katika vita ambavyo vimegharimu maisha ya maelfu ya watu na mamilioni kuwa wakimbizi.

Tangu kuanza kwa vita, pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia na kulipua mabomu maeneo ya makazi bila kujali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *