Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Hamis Tabasamu amesema watu waliokuwa wakiuvuka Mto Pangani katikati ya miaka ya 1980 watakubali kuwa Tanzania inajengwa kwa kasi kutokana na ujenzi wa daraja la kudumu lenye urefu wa mita 525.
Kauli hiyo imetolewa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipokagua ujenzi wa daraja hilo na barabara ya lami kutoka Tanga hadi Pangani yenye urefu wa Kilometa 50 huku wajumbe wa kamati hiyo wakipongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema “Tanzania ni kama construction site”.
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)