‎#HABARI: Afisa Usafirishaji mkoani Tabora, aliyetambulika kwa jina la Kimwaga Rashid Kimwaga (40), ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Usule, Kata ya Mbugani.

Katika tukio hilo wauaji hao walitega waya wenye ncha kali uliosababisha majeraha kwa waendesha pikipiki wengine wawili, huku wakijaribu kupora pikipiki bila mafanikio baada ya polisi na raia wema kufika katika eneo hilo haraka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika waliokuwa wakitekeleza matukio hayo.

Kamanda Abwao ameahidi kutoa taarifa kamili hivi punde kuhusu maendeleo ya msako huo, huku hali ya tahadhari ikiongezeka miongoni mwa wasafirishaji mkoani humo kufuatia shambulio hilo la kinyama.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *